Swahili

Kila mtu ambaye alipoteza mawasiliano na familia kwa sababu ya vita, maafa ya asili au viwanda, mgogoro wa kibinadamu au kwa sababu ya uhamiaji, anaweza kuomba usaidizi kwa Shirika la Msalaba Mwekundu kujaribu kupata mawasiliano  na mtu wake. Hii duniani kote wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu, wanajitahidi kurejesha mahusiano ya familia kuhusu mtu (watu) ambaye wamepoteyana.

Katika hali hii, Shirika la Msalaba Mwekundu ya Ubelgiji inaweza kukusaidia:

  • kutafuta watu (familia yako ) ikiwa wamepotea;
  • kubadilishana ujumbe na marafiki na familia wakiwa katika mazingira ambapo vyombo vya habari zilioathirika     au zilioingiliwa;
  • kuwa tena na wapendwa ambao walikutwa na Shirika la Msalaba Mwekundu na uwezo wa kunufaika na kuungana kwa familia.

Shirika la Msalaba Mwekundu ya Ubelgiji pia inaweza:

  • kukusaidia kufafanua hatma ya mpendwa, ambae bila shaka amekwenda wakati wa vita ya kale ( hadi Vita Kuu ya Pili);
  • kukutumia hati ya kukamatwa (kwa sharti kwamba Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu - ICRC - ilikutembelea ulipokuwa gerezani);
  • kuzuia shiida ya kuvunja kuwasiliana tukikupa habari sahihi kulingana na hali ya wazi.

Kila ombi itabebwa juu ya kesi na kesi, juu  ya msingi na kulingana na vigezo ambazo zinaweza kutofautiana kulingana na nchi, asili ya hasara ya kuwasiliana, kama au si vita...

Tovuti hizi mbili zimejitolea kutafuta kwa ajili ya kukosa watu

Shirika la Msalaba Mwekundu pia ina tovuti mbili amazo imetolea kutafuta watu waliopotea.

Moja inahusu maalum ya watu wamekosekana wakati wa njia zao kwenda Ulaya na watu wanaohama ndani ya Ulaya. Unaweza tayari kuona tovuti hii ambayo inaonyesha picha za wale ambao wanaotafuta mpendwa.

Nyingine imejitolea kutafuta watu waliopotea wakati wa vita na kutafuta watu waliopotea wakati wa majanga ya hivi karibuni. Kupitia tovuti hii, watu ambao wamepoteyana wanaweza kukutana na kubadilishana mawasiliano ya habari. Hivi sasa, nchi zinazohusika ni : Bosnia, Croatia, Philippines, Kosovo, Nepal na Somalia.

Usisite kuwasiliana na sisi / Kurejesha maasiliano na familia.

Kama maombi yako anafaa vigezo zetu, Huduma la Msalaba Mwekundu inakukaribisha na inakusaidia katika jitihada yako.

Kama huna kuzungumza Kifaransa, Kiholanzi au Kiingereza, tunaweza kutabiri mbele ya mkalimani. Unaweza pia kuanzisha mwenyewe katika kampuni mtu ambaye unaaminia il akutafsirie.

Wakati wa mkutano wetu na wewe, tunakueleza zaidi kuhusu kazi yetu na tunajaza fomu pamoja na wewe. Hii fomu inapelekwa na Shirika la Msalaba (Croix-Rouge / Croissant-Rouge au CICR) nchini ambayo unadhani familia yako. Uko nchini, wenzetu watafanya hatua ya kurejesha uhusiano kati ya wewe na mtu ambae unatafuta.

Mara baada ya kupata taarifa kuhusu wewe,  tutaasiliana na wewe. Uwezo wetu wa kupata watu inategemea: hali za mitaa ( rasilimali watu , vifaa, ...) pamoja na hali ya usalama ya nchi husika. Sisi hatuwezi kutoa maoni juu ya muda wa utafutaji juu kwamba wakati mwingine muda huu kua mrefu sana.

Huduma zetu zote ni bure na kila kesi inatibiwa kwa siri.

 

Download the PDF

For more information: